SERIKALI Mkoani TABORA imewataka wawekezaji katika kiwanda cha Nyuzi cha TABORA kurejesha kiwanda hicho mikononi mwa serikali kutokana na kushindwa kukiendesha kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na kuwakosesha wananchi ajira.
Akizungumza katika ziara ya kushitukiza kiwandani hapo, Mkuu wa Manispaa ya TABORA, Bwana SULEIMAN KUMCHAYA amesema kufuatia wamiliki wa kiwanda hicho kutoka INDIA kushindwa kukiendesha,iko haja ya kukirudisha mikononi mwa serikali.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la TABORA mjini, Mheshimiwa EMMANUEL MWAKASAKA aliyefuatana na mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha kufungwa kiwanda hicho ambacho sasa kimegeuka kuwa hifadhi ya wanyamapori kama vile tumbili badala ya kuzalisha na kutoa ajira kwa vijana.