BUNGE la Burundi leo linajadili mpango wa Umoja wa Afrika kutuma kikosi cha wanajeshi wa kuwalinda raia nchini humo, ambao tayari serikali imeukataa na kukitaja kikosi hicho kuwa ni cha uvamizi.
Wabunge wanatarajiwa kupinga kuletwa kwa kikosi hicho, kilichopendekezwa na Umoja wa Afrika wiki iliyopita, wakati ambapo wasiwasi unazidi kuhusu kuongezeka kwa machafuko katika taifa hilo dogo.
Chama tawala cha CNDD-FDD kimesema lengo la kikao hicho kisicho cha kawaida kilichotarajiwa kutangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni za Umma, ni kuwapa sauti raia kupitia wawakilishi wao.