SERIKALI WIlayani Chunya Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa maji wilayani humo.
Hatua hiyo imekuja kufuataia kampuni ya Peak Resource inayojihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya ardhi katika kata ya ngwala wilayanii chunya mkoani mbeya kuchimba visima viwili vya maji vyenye thamani ya shilingi milioni 16.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya visima hivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Elias Tarimo amesema hatua ya kampuni hiyo kuamua kuchimba visima hivyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ni jambo jema na linalotakiwa kuungwa mkono na wananchi hao.