SHIRIKA la kutetea haki za Binadamu Duniani la Amnesty International, limeituhumu serikali ya Burundi kwa mauaji ya watu wasio na hatia na matumizi mabaya ya Jeshi la nchi hiyo.
Aidha limelaani mauaji yaliyotokea Disemba 11 mwaka huu ambapo watu nane waliuawa wakati jeshi la serikali lilipokuwa likijihami dhidi ya mashambulizi ya waasi watatu waliovamia vituo vitatu tofauti vya Jeshi.
Hata hivyo Serikali ya Burundi imeeleza kwamba wale waliouawa ni maadui, ingawa maelezo hayo yamepingwa vikali na Amnesty ambao wamesema kuwa wengi wa waliouawa ni watu wasio na hatia na raia wa Taifa hilo.