KUFUATIA kukithiri kwa uchafu katika kata ya Upanga Magharibi licha ya kuwepo kwa kampuni ya TIRIMA iliyochukuwa tenda ya kufanya usafi katika kata hiyo, Uongozi umekusudia kuvunja mkataba na kampuni hiyo.
Diwani wa kata ya Upanga Magharibi Adinani Kitwana Kondo amesema eneo lililopo hospitali ya Muhimbili limekithiri kwa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya watu wengi wanaoishi na wanaotembelea maeneo hayo.
Kondo amesema kampuni hiyo ya TIRIMA imekuwa ikikusanya shilingi elfu kumi na tano kwa kila mkazi wa eneo la Upanga bila kutekeleza wajibu huo wa kufanya usafi jambo ambalo amesema ni sawa na kuwatapeli wananchi hivyo hakuna sababu ya kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo.