BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LAPOKEA MIGOGORO 41 NA KUIPATIA UFUMBUZI 2015

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LAPOKEA MIGOGORO 41 NA KUIPATIA UFUMBUZI 2015

Like
225
0
Wednesday, 30 December 2015
Local News

BARAZA la Taifa la Ujenzi limepokea migogoro 41 na kufanikiwa kuitafutia ufumbuzi katika kipindi cha mwaka 2015 kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Ujenzi nchini.

 

Hayo yamesemwa leo na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo,  Mhandisi Dokta Leonard Chamuriho  wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.

 

Akizungumzia majukumu ya Baraza hilo katika kutatua Migogoro inayojitokeza katika Sekta hiyo, Mhandisi Chamuriho amebainisha kuwa migogogoro iliyojitokeza imekuwa ikitegemea Ukubwa wa mradi, Hali ya eneo la mradi, Ubora wa kazi, uelewa wa vipengele mbalimbali vya mkataba katika mradi husika na moja ya pande zinazohusika kukatisha mkataba.

 

Comments are closed.