KUFUATIA Manispaa ya kinondoni kukabiliwa na tatizo la upumgufu wa shule za sekondari lililosababishwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanao faulu, Manispaa hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu imepanga kujenga shule sita ili kusaidia kupunguza sehemu ya tatizo hilo.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni PAUL MAKONDA amesema ni aibu kubwa kwa manispaa kubwa kama ya hiyo kuwa na upungufu wa shule za sekondari kutokana na manispaa hiyo kuwa na wadau wengi wenye uwezo wa kusaidia kuondoa tatizo hilo.
MAKONDA ameongeza kuwa ujenzi wa shule hizo utahusisha zaidi ya kata sita na unatarajiwa kuchukua zaidi ya miezi mitatu kukamilika.