SIKU moja baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la haidrojeni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza mikakati ya kuiwekea vikwazo.
Hata hivyo baadhi ya Wataalamu wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la sasa la nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika mwongo mmoja, wakisema huenda lisiwe la haidrojeni kutokana na mlipuko uliotokea.
Bomu la hydrojeni ni moja ya mabomu hatari ya jamii ya atomiki au nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu hili la hydrojeni lina uwezo mkubwa kiasi kwamba linaweza kulipua mji mmoja wote kwa mlipuko mmoja.