RAIS MAGUFULI AMPONGEZA SAMATTA

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA SAMATTA

Like
230
0
Friday, 08 January 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu  Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria jana usiku.

 

Mhe. Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.

Comments are closed.