BALOZI wa Uingereza nchini ameahidi kuisaidia Halmashauri ya kinondoni katika kutatua kero ikiwemo kero ya mafuriko pamoja na kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu ,sekta ya afya na michezo.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es alaamu na mkuu wa wilaya ya kinondoni PAUL MAKONDA mara baada ya kumaliza mazungumzo na balozi huyo, DIANA MELYROSE ambapo amesema kutokana na kuwepo na changamoto mbalimbali katika manispaa ya kinondoni manispaa hiyo imekuwa na mazungumzo na baadhi ya wadau wa halmashauri ya kinondoni wakiwemo mabalozi ili kutafuta namna ya kuweza kutatua changamoto hizo .