RAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir kwa mara ya kwanza amewaomba radhi raia wa nchi hiyo kutokana na mateso na dhiki ambayo wamepitia wakati wa mzozo wa kisiasa uliodumu miaka miwili.
Rais Kiir amesema kuomba msamaha ndiyo hatua ya kwanza katika kufanikisha maridhiano nchini humo.
Amechukua hatua hiyo wakati wa kufungua rasmi mkutano mkuu wa chama tawala cha SPLM. Jana, pande zilizohusika katika mzozo huo ziliafikiana kuhusu kugawana nyadhifa za uwaziri katika baraza la mawaziri la serikali ya umoja.