WAFANYABIASHARA wa soko lisilo rasmi lililopo tegeta kwa ndevu Jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum la kufanyia biashara zao kutokana soko la nyuki lililotengwa kuwa finyu hali inayosababisha wao kuendelea kuwepo sokoni hapo.
Wakizungumza na efm Jijini Dar es salaam Wafanya Biashara hao wamesema kuwa kipinndi cha nyuma eneo hilo lilikuwa lipo chini ya serikali ya mtaa ambapo kwa sasa linamilikiwa na mtu binafsi ambae ndie amewapangisha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Soko hilo RAMADHAN HUSSEN amesema kuwa eneo la nyuki liliotengwa kwaajili ya wafanya biashara hao ni eneo la boko na siyo Tegeta ambapo pia ameshawahi kuongea na serikali ya mtaa huo kuhusu eneo hilo kulifanya liwe rasmi kwaajili ya wafanyabiashara kufanya biashara zao lakini mpaka sasa suala hilo halijafanikiwa.