SOMALIA: MASHAMBULIZI YA HOTELI YAUA 20

SOMALIA: MASHAMBULIZI YA HOTELI YAUA 20

Like
252
0
Friday, 22 January 2016
Global News

WAZIRI wa Mambo ya Usalama wa Ndani nchini Somalia amesema watu 20 wamefariki baada ya hoteli mbili maarufu za ufukweni kushambuliwa mjini Mogadishu.

Waziri Abdirisak Omar Mohamed ameviambia vyombo vya habari kuwa watu wengine 20 wamejeruhiwa baada ya hoteli za Lido Sea Food na Beach View kushambuliwa jana jioni.

Hata hivyo tayari Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabaab limekiri kuhusika kwenye shambulio hilo ambalo limetajwa kuwa ni miongoni mwa mashambulio ya kikatili.

Comments are closed.