MAKABURI YA WATU WENGI YAGUNDULIKA BURUNDI

MAKABURI YA WATU WENGI YAGUNDULIKA BURUNDI

Like
221
0
Friday, 29 January 2016
Global News

SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema limeona picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi.

Amnesty limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura.

Shirika hilo limeongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku ya tarehe 11,Desemba,siku ambayo ilishuhudia machafuko makubwa mjini Bujumbura.

Comments are closed.