SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) leo linafanya mkutano wa dharura kujadili kuenea kwa virusi vya Zika.
Mkutano huo mjini unaofanyika Geneva utajadili iwapo mlipuko wa virusi hivyo unafaa kutangazwa kuwa dharura ya kimataifa.
Katika matukio mengi, watu walioambukizwa virusi hivyo vya Zika huwa hawaonyeshi dalili zozote, lakini virusi hivyo vinadaiwa kusababisha maelfu ya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo Amerika Kusini.