UMOJA wa Afrika umeamua utapeleka ujumbe maalum nchini Burundi kujaribu kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuridhia jeshi la kulinda amani baada ya rais Nkurunzinza kuipinga hatua hiyo.
Taarifa hizo zimetolewa na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika baada ya kumalizika mkutano wa kilele wa Umoja huo hapo jana.
Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka nchi za Magharibi aliyefuatilia mkutano wa jana ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba viongozi wa Umoja wa Afrika waliokutana kwa siku mbili pia huenda wakalitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuishinikiza Burundi kwa kutangaza uwezekano wa kuiwekea vikwazo ikiwa nchi hiyo itaendelea kukaidi hatua ya kupelekwa jeshi la Umoja wa Afrika la kulinda amani.