SERIKALI imejipanga kuhakikisha inaboresha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchini ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa.
Akijibu swali la Mheshimiwa Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF), leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya masikini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika.
Aidha Mheshimiwa Kairuki amesema kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizo zinantolewa na Serikali ili kusaidia Kaya masikini ziweze kujikwamua kiuchumi.