RAIS wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud ametoa maelezo kuhusu idadi ya wanajeshi wa Kenya waliofariki kufuatia shambulio la al-Shabab katika kambi yao huko el-Adde mwezi uliopita.
Rais huyo ametoa idadi hiyo kuwa kati ya wanajeshi 180 na 200 katika mahojiano na runinga moja ya Somali ,Cable TV.
Wapiganaji hao wa al-Shabab wamesema kuwa wanajeshi 100 walifariki na Kenya bado haijatoa idadi yoyote ya wanajeshi wake waliofariki.