MKUU wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utoaji wa misaada ya kibinaadamu, Stephen O’Brien, amesema shirika la Mpango wa Chakula duniani, WFP, limedondosha chakula kutoka angani katika mji wa Deir el-Zour, ambao umekuwa ukizingirwa na kundi la Dola la Kiislamu.
O’Brien ameliambia baraza la usalama la umoja huo mjini New York kwamba tani 21 za msaada zilidondoshwa.
Hata hivyo msemaji wa WFP Bettina Luescher amesema katika taarifa yake kwamba operesheni nzima ilikabiliwa na changamoto za kiufundi.