UMOJA WA ULAYA UMEELEZEA WASIWASI WAKE JUU YA UKANDAMIZAJI UNAOENDELEA KWENYE MPAKA WA UGIRIKI NA MACEDONIA

UMOJA WA ULAYA UMEELEZEA WASIWASI WAKE JUU YA UKANDAMIZAJI UNAOENDELEA KWENYE MPAKA WA UGIRIKI NA MACEDONIA

Like
233
0
Wednesday, 02 March 2016
Global News

UMOJA wa Ulaya umeelezea wasiwasi wake kuhusu ukandamizaji unaoendelea kwenye mpaka wa Ugiriki na Macedonia, ambako polisi wa Macedonia waliwafyatulia mabomu ya kutoa machozi mamia ya wahamiaji.

Msemaji wa halmashauri kuu wa umoja huo Margaritis Schinas, amesema matukio yalioonyeshwa kwenye mpaka huo siyo njia sahihi ya kushughulikia mgogoro huo.

Naye Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema matukio hayo yanaonyesha umuhimu wa mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa ya umoja wa Ulaya wa kujadili mgogoro wa wakimbizi.

Comments are closed.