KAMISHENI ya Umoja wa Ulaya imeidhinisha makubaliano kati ya Umoja huo na Ugiriki juu ya ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Azerbaijan unaolenga kupunguza utegemezi wa nishati kwa Urusi.
Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 878, litasafirisha mita bilioni 10 za ujazo za gesi kwa mwaka kutoka Azerbaijan hadi Italia kupitia Ugiriki, Albania na Bahari ya Adriatiki.
Awamu ya kwanza ya gesi hiyo inatazamiwa kuwasili barani Ulaya mwaka 2020 ambapo Ugiriki itafaidika kwa mafao ya kodi kwa miaka 25.