KOREA KASKAZINI imerusha makombora mawili ya masafa mafupi kuelekea Bahari ya Japan, kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini.
Mkuu wa majeshi wa Korea Kusini amesema makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 500 kutoka kusini mwa Korea Kaskazini, kabla ya kuangukia pwani ya mji wa kusini mashariki mwa Japan, mapema leo.
Tayari Japan imetuma rasmi malalamiko yake dhidi ya Korea Kaskazini kupitia ubalozi wake uliopo mjini Beijing, China, kwa mujibu wa shirika la habari la Japan, Kyodo. Korea Kaskazini imechukuwa hatua hiyo siku chache kabla ya kuanza kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini hapo Jumatatu, inayodai kuwa ni maandalizi ya uvamizi dhidi yake.