WAZIRI MKUU AAGIZA CAG KUKAGUA MAMLAKA YA BANDARI TPA

WAZIRI MKUU AAGIZA CAG KUKAGUA MAMLAKA YA BANDARI TPA

Like
238
0
Tuesday, 22 March 2016
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali –CAG-aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akakague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.

 

Mheshimiwa Majaliwa ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji wao wa kazi.

 

Mbali na hayo amesema kuwa kuna dalili za kutupiana lawama baina-TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyokuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekani na imedaiwa kuwa wakala hajalipia mzigo wakati alishaulipia.

Comments are closed.