JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata pikipiki 519 ambazo zimekuwa zikitelekezwa kutokana na makosa mbalimbali ya barbarani kutoka katika manispaa tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kamanda wa kanda maalumu ya mkoa huo kamishina Simon Sirro amesema katika kuhakikisha wanapambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo wa kutumia pikipiki jeshi hilo limefanikiwa kuzuia pikipiki nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitelekezwa na baadhi ya watuhumiwa.
Kamishina Sirro ameongeza kuwa licha ya oparesheni hiyo kufanikisha kukamtwa kwa pikipiki hizo pia wamefanikiwa kukamata gari moja la wizi na marobota 10 ya vitenge na katoni 17 ya pampers ambayo yalikuwa yakitoroshwa kwa ajili ya kukwepa kodi.