IMEELEZWA kuwa endapo sekta ya viwanda itasimamiwa na kuwekewa mazingira bora, ina nafasi kubwa ya kuleta mabadaliko na kuweza kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuliwezesha Taifa kufika pale linapokusudia kufika kama inavyoainishwa na dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa REPOA Dokta Donald Mmari katika mahojiano maalum na Efm juu ya namna sekta ya viwanda inavyoweza kutumika kuleta mageuzi ya kiuchumi yanayoenda sanjari na mabadiliko ya mtu mmoja mmoja.
Dokta Mmari amesema kuwa licha ya kuwa uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia saba upunguaji wa umasikini umekuwa ukipungua kwa asilimia ndogo hali inayowafanya Wananchi kutoona ukuuaji wa uchumi kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa ya uhaba wa ajira.