WENGER AONYESHA HOFU EPL

WENGER AONYESHA HOFU EPL

Like
270
0
Monday, 25 April 2016
Slider

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema ameanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.

Anasema wasiwasi zaidi unatokana na hatari ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 19.

The Gunners walipoteza nafasi ya kupanda hadi nambari tatu kwenye jedwali baada ya kutoka sare tasa na Sunderland ugenini Jumapili.

“Tuna haja sana na hilo na tuna wasiwasi kuhusu hilo kwa sababu sasa yatakuwa ni mapambano,” alisema Wenger kuhusu juhudi za kutaka kumaliza katika nne bora.

“Inasikitisha kwa sababu sisi hucheza ili tushinde taji la ligi na hali kwamba hatutashindi inauma.”

Arsenal, hawajamaliza nne ya nne bora Ligi ya Premia tangu msimu wa 1995-96.

Kwa sasa wamo alama 12 nyuma ya viongozi Leicester City wakiwa wamesalia na mechi tatu za kucheza.

Wamo alama tano pekee juu ya Manchester United walio nambari tano, na ambao wana mechi moja hawajacheza.

Arsenal wamepangiwa kukutana na Norwich 30 Aprili nyumbani, Manchester City 8 Mei ugenini na Aston Villa 15 Mei nyumbani.

Manchester United nao watakuwa nyumbani dhidi ya Leicester 1 Mei na ugenini dhidi ya Norwich and Westham 7 Mei na 10 Mei mtawalia.

Watamaliza msimu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Bounemouth tarehe 15 Mei.

Comments are closed.