KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI KUFANYIKA IJUMAA WIKI HII

KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI KUFANYIKA IJUMAA WIKI HII

Like
260
0
Wednesday, 27 April 2016
Local News

KITUO cha Uwekezaji Tanzania –TIC, kwakushirikiana na Russian Export Club kimeandaa Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

 

Mbali na TIC kongamano hilo limeandaliwa pia kwa ushirikiano na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Wakati wa Kongamano hilo, yatafanyika majadiliano ya moja kwa moja na mikutano ya Biashara-kwa-Bisahara, mikutano ya Serikali na Wafanyabiashara na Serikali kwa Serikali .

Comments are closed.