IMEBAINISHWA kuwa kwa mwaka 2012/2015 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imechangia zaidi ya shilingi bilioni 3 katika pato la taifa ambayo ni sawa na asilimia 2 ya pato la Tanzania.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam katika tathmini iliyofanywa na KPMG juu ya mchango mpana wa kiuchumi na kijamii ikiwamo ukuzaji wa uchumi,ajira,na kupunguza umaskini,tathmini iliyofanyika kuhusu mtaji na shughuli za uwekezaji kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/ 2015.