MGOMO wa wafanyakazi wa sekta ya umma umevuruga shughuli za kawaida nchini Ujerumani hii leo.
Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya umma Verdi wamegoma kufanya kazi kutokana na madai ya nyongeza ya mshahara.
Viwanja vya ndege vya Frankfurt, Dusseldorf na Munich vimeathirika na mgomo huo ikiwa ni pamoja na usafiri wa mjini katika miji mbali mbali, lakini uwanja wa ndege wa mjini Berlin unafanyakazi kama kawaida.