MJUMBE wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amezitaka Urusi na Marekani kuimarisha usitishaji tete wa mapigano nchini Syria kabla ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza miaka 5 ya mzozo nchini humo.
Kauli hiyo ya de Mistura inakuja muda mfupi baada ya kulifahamisha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mazungumzo ya amani, ambayo amesema yamepiga hatua licha ya vikwazo vya hivi karibuni.