TAMA YATAKA MITAALA YA UTOAJI WA MAFUNZO YA UKUNGA KUFANYIWA MAREKEBISHO

TAMA YATAKA MITAALA YA UTOAJI WA MAFUNZO YA UKUNGA KUFANYIWA MAREKEBISHO

Like
268
0
Friday, 29 April 2016
Local News

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetakiwa kurekebisha mtaala wa kutoa mafunzo ya ukunga ili kuifanya taaluma hiyo iweze kuheshimika na kunusuru maisha ya watoto na akina mama wakati wa kujifungua.

Wito huo umetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA-Dokta. Sebalda Leshabari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Semina maalumu iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema Wizara hiyo inatakiwa kuangalia namana ya kurekebisha mitaala ya utoaji wa mafunzo ya ukunga kutokana na fani hiyo kuonekana ikitolewa kiholela.

Comments are closed.