HUYU NDIO SHABIKI ATAKAEKUWA MILIONEA IWAPO LEICESTER CITY ITATWAA UBINGWA WA EP

HUYU NDIO SHABIKI ATAKAEKUWA MILIONEA IWAPO LEICESTER CITY ITATWAA UBINGWA WA EP

Like
334
0
Friday, 29 April 2016
Slider

Shabiki mmoja wa timu ya Leicester amesema kuwa ana uhakika klabu hiyo itashinda ubingwa wa ligi na kumfanya kupata zaidi ya pauni 20,000 ambayo ni sawa na milioni 64 za Tanzania.

Leigh Herbert aliwekeza 5000 baada ya kupata vinywaji kadhaa wakati wa likizo huko Newquay ,Cornwall mwaka uliopita.
Nina furaha tele kwa sababu nina uhakika wa asilimia 100 kwamba hilo litafanyika.

Leigh aliweka fedha alicheza kamari hiyo kufuatia uteuzi wa mkufunzi Claudio Ranieri.Nilifikiria kwamba atailetea kilabu hiyo kitu maalum.

Nilijua kwamba kutokana na uzoefu alionao kuna kitu kitafanyika.Na kulingana na mambo yalivyo kwa sasa Leigh alikuwa na haki kuwa na matumaini.

Iwapo timu yake itaishinda Manchester United ama Spurs ishindwe na wapinzani wake wa jadi Chelsea wikendi hii,Leicester watakuwa mabingwa na Leigh atajipatia pauni 20,000.

Comments are closed.