WAZIRI wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amefungua siku ya pili ya mazungumzo mjini Geneva yenye lengo la kutafuta njia ya kupata suluhu ya mapigano nchini Syria.
Kerry amekutana na Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia Adel Al-Jubeir na anapanga pia kuwa na mazungumzo baadae na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Syria Staffan De Mistura.
Waziri Kerry amesema hatua za maelewano kuhusu njia ya kupunguza mashambulizi mjini Aleppo zinaendelea kuimarika, lakini kazi ya ziada inahitajika.