ILALA: POLISI YAWATOA HOFU WANANCHI JUU YA HALI YA USALAMA

ILALA: POLISI YAWATOA HOFU WANANCHI JUU YA HALI YA USALAMA

Like
284
0
Thursday, 05 May 2016
Local News

JESHI la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala na kuachana na taarifa za uvumi kuwa hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi sio nzuri.

 

Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Lucas Mkondya amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote.

 

Kuhusiana na malalamiko ya wananchi wa Buguruni kuhusiana na kuwepo kwa kundi la vibaka na waporaji kamanda Mkondya amesema kuwa Jeshi lake linaendelea na operesheni ya kukamata wahalifu usiku na mchana ili kuhakikisha Mkoa huo unakuwa salama.

Comments are closed.