MUFTI Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber bin Ally amewataka watanzania kudumisha umoja na mshikamano ili kujenga taifa na kuleta maendeleo.
Sheikh Zuber ameyasema hayo wakati akizungumza na baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA katika semina elekezi kwa viongozi wa baraza hilo Taifa.
Naye Sheikh mkuu wa mkoa wa Mtwara Nurdin Abdala Athumani ameongeza kuwa watanzania ili wapate maendeleo ni lazima watumie viwanda ipasavyo kuzalisha na kudumisha suala la umoja pamoja na amani iliyopo kwa manufaa ya Taifa.