KATIKA kutekeleza agizo la serikali la kuwafikia wateja laki 4 ifikapo June mwaka 2016 Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) limesema linaendelea na zoezi la uunganishaji wa huduma ya
Maji kwa wananchi wote wa jiji la Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa kwenye awamu hii ya zoezi la uunganishaji wateja wapya shirika litagharamia gharama zote za maunganisho ambazo ni gharama za uunganishaji mabomba na vifaa vya uunganishaji.