WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA VYEMA

WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA VYEMA

Like
279
0
Tuesday, 24 May 2016
Local News

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wametakiwa kushirikiana vyema ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuharakisha maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.

 

Wito huo umetolewa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar na kusema kuwa utendaji mzuri wa viongozi hao ndani ya Baraza hilo ndiyo utakaoweza kukirahisishia kazi Chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

 

Akifafanua suala hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema ushirikiano baina yao pia utaongeza ufanisi wa kusimamia vyema shughuli za baraza kulingana na mahitaji ya wananchi majimboni.

Comments are closed.