BRAZIL: MKANDA WA VIDEO WAMUUMBUA WAZIRI

BRAZIL: MKANDA WA VIDEO WAMUUMBUA WAZIRI

Like
289
0
Tuesday, 24 May 2016
Global News

WAZIRI wa mipango wa serikali mpya ya Brazil amewekwa pembeni baada ya kukutwa katika mkanda wa video akifanya njama ya kukwamisha uchunguzi mkubwa wa nchi hiyo unaohusu ufisadi.

Katika rekodi ya kanda hizo, ambazo zimetolewa na gazeti moja nchini humo, waziri Romero Juca, ameonekana akisema kuwa kuondolewa madarakani kwa Rais Dilma Rousseff, kutazuia kuchunguzwa kwa kampuni ya serikali ambayo ni kubwa katika uzalishaji wa mafuta, Petrobras.

Hata hivyo, waziri huyo amesema kauli yake hiyo imeeleweka vibaya na kwamba anaunga mkono uchunguzi dhidi ya ufisadi.

Comments are closed.