KOREA Kaskazini imefanya jaribio lingine la makombora yake ya masafa marefu katika eneo la mashariki ya pwani yake lakini linaonekana kufeli.
Wakizungumzia makombora hayo wanajeshi wa Korea Kaskazini wamesema kuwa haijulikani ni kombora gani limefeli na kwamba hiyo imejirudia baada ya makombora mengine yaliyojulikana kwa jina la ”Musudan” kufeli mnamo mwezi Aprili.
Hata hivyo imeelezwa kutanda kwa wasiwasi katika eneo hilo baada ya Pyongyang kujaribu kombora la nne la Kinyukia mnamo mwezi Januari pamoja na makombora mengine.