Baada ya kukabidhi magari mawili na pikipiki kumi kwa wasikilizaji wake kupitia
shindano la shikandinga , EFM redio inakuja na donge nono kupitia mchezo wa
sakasaka ambao huchezeshwa kila mwaka toka kituo kianzishwe.
Saka saka ni shindano ambalo efm redio huficha kitu katika eneo fulani ambapo msikilizaji hupewa maelekezo yake hivyo atatakiwa kwenda katika eneo
hilo na kukitafuta hicho kitu kulingana na shindano.
Mwaka huu mchezo wa sakasaka utaanza tarehe 12/06/2016, utachezeshwa katika
wilaya tano (5) ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Mkuranga, na Kisarawe
ambapo jumla ya kiasi cha milioni tatu (3) kushindaniwa katika kila wilaya.
Ili kuweza kushiriki katika mchezo huu jamii inapaswa kusikiliza kwa makini
vipindi vya redio ambapo atapata dondoo za jinsi mchezo utavyokua ukichezwa
Lengo madhubuti la mchezo huu ni kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine
kwani pesa ambazo watajishindia zitawasaidia katika maisha yao kiujumla kama
biashara, familia, elimu, n.k
“Idadi kubwa ya wasikilizaji wetu wana changamoto nyingi za maisha hivyo kama
redio tunawawezesha kwa kupitia vitu tofauti tofauti ambavyo vitawasaidia
kujikwamua kimaisha”