Maisha ya mlinzi wa kati wa Liverpool Mamadou Sakho yanaonekana kuanza kuwa magumu baada ya kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp kuamuru nyota huyo arudi nchini England kutoka Calfonia Marekani ambapo timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya nchini England inayoanza kutimua vumbi mwezi ujao.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya uingereza kocha Jurgen Klopp hajafurahishwa na mwenendo wa kitabia wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kwenye kambi yao huko Marekani nakuagiza arudi England.
Sakho alianza kukorofishana na kocha Jurgen Klopp juma lililopita baada ya kuchelewa wakati wanajiandaa kupanda ndege kuelekea Marekani.
Mbali na hilo pia Sakho anareporiwa kuingilia mazungumzo ya kocha huyo na website ya klabu vitu ambavyo vitatajwa kumkera sana kocha huyo wa Kijerumani.