Rais wa Ufaransa Francois Hollande amepuuzilia mbali hatua ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kukosoa sera ya Ujerumani kuhusu wahamiaji barani Ulaya.
Bw Hollande alisema hatua hiyo ya Bw Trump si ya busara.
“[Ulaya] haihitaji ushauri kutoka nje, kuambiwa inafaa kufanya nini,” Bw Hollande alisema.
Bw Trump alikuwa amesema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alifanya “kosa kubwa” kwa kuwaruhusu wahamiaji kuingia nchini mwake kwa wingi.
Bi Merkel kwa upande wake, akijibu tamko hilo la Trump, alisema bara Ulaya linafaa kuachwa lijifanyie maamuzi.