Rais John Magufuli amewataka watendaji wanaosimamia mradi wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam (Dart) kuhakikisha unaingiza faida kinyume na hapo hasara itakuwa kwao.
Aidha, Rais Magufuli aliwataka mawaziri wanaosimamia mradi huo, George Simbachawene (Tamisemi) na Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi) kumpatia taarifa inayoeleza kiasi cha fedha kilichoingia tangu mabasi hayo yaanze kufanya kazi.