Binti mmoja wa Kipalestina aliyekamatwa baada ya kumchapa kofi mwanajeshi, Msichana huyo Ahed Tamimi alikiri kuwa na hatia kwa makosa manne aliyokuwa akishtakiwa kati ya 12 yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo shambulio la mwili, wakili wake ameeleza.
Kadhalika, atalipa faini ya shekeli 5,000 sawa na dola 1,440 .
Binti huyo mwenye miaka 17 alikamatwa baada ya kunaswa kwenye picha ya video akiwakabili wanajeshi wawili nje ya nyumba yake mwezi Desemba.
Uamuzi wa mahakama unamaanisha kuwa ataachiwa huru kipindi cha majira ya joto kwa sababu hukumu yake imehesabu siku alizokaa korokoroni, mwanasheria wake Gaby Lasky amenukuliwa na shirika la habari la AFP.eshi wa Israel amekiri kosa na atatumikia kifungo cha miezi minane gerezani kufuatia maafikiano kati yake na upande wa mashtaka.