Uturuki yaondoa hali ya hatari

Uturuki yaondoa hali ya hatari

Like
445
0
Thursday, 19 July 2018
Local News

Vyombo vya habari vya taifa nchini Uturuki vimetangaza kwamba
serikali imeondoa hali ya hatari iliyowekwa nchini humo kufuatia
mapinduzi yaliyoshindwa miaka miwili iliyopita.
Katika kipindi hicho makumi kwa maelfu ya watu walikamatwa na
kushikiliwa bila ya kufunguliwa mashtaka chini ya agizo la Rais wa
nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.
Wanajeshi, Polisi, Raia, Waandishi wa Habarai na walimu ni
miongoni mwa waliokamatwa.
Maelfu wengine ikiwemo majaji kadhaa waliachishwa kazi zao.
Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema
kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari pekee hakuwezi kbadili hatua
kazli za kisiasa zilizochukuliwa ambazo ziliibadili nchi hiyo na
kuifanya inayokandamiza haki za binadamu.
Mapema mwezi huu Rais Erdogan aliapishwa kuwa Rais wa nchi
hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, wagombea wa upinzani walisema
kuwa kitu cha kwanza watakachokifanya iwapo watashinda
uchaguzi ni kumaliza amri hiyo ya hali ya hatari iliyowekwa.
Wengi ya waliokamatwa kipindi hicho ni wale waliokuwa
wakidaiwa kuwa wafuasi wa mpinzani wa Rais Erdogan anayeishi
uhamishoni nchini Marekani, Fethullah Gulen, ambaye awali
alikuwa mshirika wa Rais wa nchi hiyo.
Uturuki ilimlaumu yeye na wafuasi wake kuwa ndio waliopanga
mapinduzi ya kutaka kuiangusha serikali ya nchi hiyo. Lakini hata
hivyo mwenyewe alikana taarifa hizo.

Reli mpya ya SGR nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *