Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB), limekana kuhusika na tuhuma za ubaguzi dhidi ya mwanasoka, Mesut Özil (29) na kusema kuwa lilipaswa kuwajibika kuhakikisha mchezaji huyo habaguliwi. Özil ametangaza kutoichezea tena timu ya taifa ya Ujerumani kutokana na kukithiri kwa vitendo na maneno ya kibaguzi dhidi yake.
Özil alishutumiwa na DFB kupitia vyombo vya habari vya Ujerumani baada ya picha akiwa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari. Mchezaji huyo wa Klabu ya Arsenal FC alishutumiwa zaidi baada ya Ujerumani kutolewa katika hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia.
DFB limekiri kwamba huenda halikulishughulikia suala hilo ipasavyo, na kuongeza kuwa linasikitisha kuwa Mesut Ozil amehisi hakulindwa vya kutosha dhidi ya kauli za kibaguzi Ujerumani haikubaliani na mwenendo wa nchi ya Uturuki hasa baada jaribio la mapinduzi kukwama. Maelfu ya watu wanashikiliwa na Serikali huku wengine wakiachishwa kazi.