Mkutano maalum kuhusu Brexit wawekwa kando kwanza

Mkutano maalum kuhusu Brexit wawekwa kando kwanza

Like
613
0
Thursday, 18 October 2018
Global News
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameamua kuuweka kando mpango wao wa kuitisha mkutano maalum juu ya mkataba wa kupeana talaka na Uingereza uliokuwa umepangwa kufanyika katikati ya mwezi ujao.

Mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungunzo na Uingereza Michel Barnier amesema pande hizo mbili  zinahitaji muda zaidi. Barnier amesema muda zaidi unahitajka ili kuweza kupiga hatua muhimu.

Kwenye mkutano wao wa siku ya Jumatano viongozi wa Umoja wa Ulaya walisema, licha ya kufanyika mazungumzo ya kina, hatua kubwa haijafikiwa ya kuwezesha kufanyika mkutano maalumu uliokuwa umepangiwa tarehe 17 na 18 mwezi ujao wa Novemba.

Wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Ulaya wamesema wataitisha mkutano wa kilele ili kuukamilisha mkataba wa kuagana na Uingereza endapo utaonekana uwezekano wa makubaliano kufikiwa.

Hapo Jumatano waziri mkuu wa Uingereza Theresa  May alitoa hotuba kwa muda wa robo saa kujaribu kuufafanua mtazamo kuhusu kuyaendeleza mazungumzo lakini  baada ya mazungumzo ya hapo awali Jumapili iliyopita  pia kushindikana. May ameripotiwa akisema kuwa pande  zote mbili zinahitaji ujasiri, hali ya kuaminiana na uongozi.

Kwa mujibu wa wanadiplomasia waziri mkuu wa Uingereza alionyesha mtazamo wa kuelewa wasiwasi wa nchi za Umoja wa Ulaya ikiwa pamoja na juu ya suala la mpaka wa Ireland ambapo nchi hiyo inapendekeza kutokuwepo vizingiti  kwenye mpaka kati ya Ireland ya Kaskazini na Jamhuri ya Ireland.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema mjini brussela kwamba nchi yake inaweza kuwatayari kurefusha muda wa mchakato wa Brexit hadi mwezi Desemba mwaka 2020 ili kuhakikisha kwamba mpaka wa nchi mbili hizo unaendelea kuwa wazi mnamo kipindi hicho.

Waziri mkuu wa Uingereza amesisitiza kuwa tarehe hiyo Uingereza na Umoja wa Ulaya zitakuwa zimeshafikia mapatano juu ya uhusiano wa kisiasa wa siku za usoni. Pendekezo hilo la kuongezea muda lilitolewa ili  kuyanasua mazungumzo. Uingereza inatarajiwa kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya mwezi Machi mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *