Waziri wa ulinzi wa Israel Lieberman ajiuzulu

Waziri wa ulinzi wa Israel Lieberman ajiuzulu

Like
550
0
Thursday, 15 November 2018
Global News

Waziri wa ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman amejiuzulu kwa ghafla akilalamika dhidi ya makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na wanamgambo wa Hamas.

Uamuzi wa kujiuzulu Avigdor Liebermann unaidhoofisha sana serikali ya mseto ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu na huenda ukapelekea uchaguzi kuitishwa kabla ya wakati. Liebermann anasema makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa pamoja na viongozi wa Gaza ni sawa na kusalim amri mbele ya ugaidi baada ya siku mbili za mapaigano makali.

Liebermann alipendelea hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya hujuma kali zaidi za makombora yanayofyetuliwa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel tangu vilipomalizika vita vya siku 50 mwaka 2014. Liebermann hakupendezewa pia na uamuzi wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu wa kuiruhusu Qatar wiki iliyopita iwapatie viongozi wa Gaza msaada wa dala milioni 15.

Sauti zimehanikiza kudai uchaguzi uitishwe kabla ya wakati. Lieberman anasema anataraji tarehe ya kuitishwa uchaguzi huo itatangazwa hivi karibuni.Vyama vya upinzani vinaunga mkono pia fikra ya kuitishwa uchaguzi kabla ya wakati. Kongozi wa chama kikuu cha upinzani -chama cha asiasav za wastani Yesh Atid ,Yaid Lapid anaashiria mwisho wa utawala wa Benjamin Netanyahu.

Serikali ya Benjamin Netanyahu ingali inadhibiti wingi wa kiti kimoja katika bunge la nchi hiyo Knesset, bila ya chama cha cha Yisrael Baiteinu cha Liebermann. Hata hivyo haitomudu madarakani hadi uchaguzi mpya uliopangwa hapo awali kuitishwa Novemba mwaka 2019.

Chama cha mkosoaji mwengine wa Netanyahu, Naftali Bennnett kimeshasema kitajitoa katika serikali ya mseto ikiwa hawatokabidhiwa wizara ya ulinzi.

Uamuzi wa Liebermann utaanza kufanya kazi masaa 48 kutoka sasa na Benjamin Netanyahu atadhibhiti wizara ya ulinzi kwa muda.Netanyahu anadhibiti pia wizara ya ammbo ya nchi za anje ya Israel.

Tangu alipotia saini makubaliano ya kuweka chini silaha, Bejamin Ntanyahu anajikuta analaumiwa kuanzia chamani na pia katika miji inaosumbuliwa na makombora ya Hamas kusini mwa Israel -ngome ya chama chake cha Likoud .Raia waalioingiwa na hasira waliteremkia majiani jana wakilalamika dhidi ya akile walichokitaja kuwa “kusalim amri serikali mbele ya visa vya matumizi ya nguvu na akushinmdwa kwake kudhamibni usalama wa kudumu. Nae msemaji wa hamas Sami Abu Zuhri anasema kujiuzulu Liebermann ni ushindi wa kisiasa kwa Gaza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *