Upinzani DRC wasema matokeo ya uchaguzi ‘hayana mjadala’

Upinzani DRC wasema matokeo ya uchaguzi ‘hayana mjadala’

Like
608
0
Wednesday, 09 January 2019
Global News

Mgombea wa urais wa upinzani nchini Congo DRC Martin Fayulu amewaonya maafisa wa uchaguzi dhidi ya ”kuficha ukweli” huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda baada ya matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa.

Bwana Fayulu amesema “watu wa Congo tayari wanajua” matokeo ya uchaguzi uliyofanyika Desemba 30 kuahirishwa kwa wiki moja.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili ya Januari 6 lakini yakaahirishwa.

Uchaguzi huo ulikuwa wa kumtafuta mrithi wa rais Joseph Kabila, ambaye anaachia madaraka baada ya kuongoza nchi hiyo ya maziwa makuu kwa miaka 18.

Kabila ameahidi kwamba uchaguzi huo ambao ulikuwa umepangwa ufanyike miaka miwili uliyopita utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini DR Congo tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.

Mrithi wake anayempendelea ambaye pia ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary,anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa upinzani Martin Fayulu,tajiri mkubwa wa mafuta na Felix Tshisekedi, mwana wa kiume wa kigogo wa upinzani.

Siku wa Jumanne, Bwana Fayulu alisema Tume ya uchaguzi (Ceni) lazima “itangaze matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais hivi karibuni,” akiongeza kuwa: “Matokeo ya uchaguzi kamwe haina mjadala.”

Awali mkuu wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa, alisema kuwa kura kutoka baadhi ya vituo vya kupigia kura bado hazijahesabiwa.

Bwana Nangaa, ambaye hajasema nilini matokeo ya awali yatatangazwa ametoa wito kwa watu kuwa na subira licha ya hali ya wasiwasi inayoendelea kushuhudiwa nchini kutokana na kucheleshwa kwa matokeo ya uchaguzi.

Huku hayo yakijiri kanisa katoliki ambalo lilitoa jumla ya waangalizi 40,000 limesema kuwa linajua ni nani aliyeshinda uchaguzi.

Tamko hilo limekosolewa vikali na maafisa wa serikali ya bwana Kabila.

Siku moja baada ya uchaguzi huduma ya mawasiliano ya intaneti yalifungwa katika miji muhimu ya taifa la DR Congo katika hatua ambayo serikali ilesema ni ya kudhibiti kusambazwa kwa matokeo ya uchaguzi amabyo sio rasmi

Mwezi uliyopita rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa wanajeshi 80 wa nchi hiyo wamepelekwa katika taifa jirani la Gabon ili kuwapa ulinzi raia wake nchini DRC endapo ghasia zitatokea baaada ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *