ABBAS MTEMVU AKABIDHIWA SHILINGI 200000 KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE

ABBAS MTEMVU AKABIDHIWA SHILINGI 200000 KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE

Like
303
0
Tuesday, 24 March 2015
Local News

JUMUIYA ya Wazazi jimbo la Temeke, wamemkabidhi Mbunge wa Temeke, ABBAS MTEMVU kiasi cha Shilingi 200,000 kwa ajili ya kuchukua Fomu ya kugombea tena nafasi hiyo ya Ubunge.

Akimkabidhi fedha hiyo kwa Niaba ya Jumuiya hiyo, Mwenyekiti SUDI MLIRO amesema kuwa hatua hiyo inatokana na ushirikiano unaofanywa na Kiongozi huyo kwa wananchi wake na kusababisha kupatikana kwa maendeleo ya haraka  ndani ya jimbo.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo,amekabidhi Pikipiki 20 kwa kila Kata katika jimbo hilo kwa lengo la kurahisisha shughuli za kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kuipigia kura ya maoni Katiba Pendekezwa pamoja na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Comments are closed.